1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kanzela Merkel ahutubia Congress

4 Novemba 2009

Heshima ya kwanza kwa Kanzela wa Ujerumani .

https://p.dw.com/p/KOBJ
Kanzela Angela Merkel akihutubia Congress.Picha: AP

Kwa mara ya kwanza Kiongozi wa serikali ya Ujerumani (Kanzela), alialikwa jana kulihutubia Bunge la Marekani-Congress- lilkijumuisha mabaraza yote 2.Hii ilikuwa heshima kubwa kwa Kanzela Angela Merkel,ambayo nae aliitumia barabara fursa hiyo kuwashukuru wamarekani kwa mchango wao katika mkesha wa kuamkia kutimu miaka 20 tangu kuanguka ukuta wa Berlin .

Wabunge waliokusanyika walibainika kuvutiwa nae:Kwani , mbele yao aliwasimamia mtu anewakilisha historia ya mafanikio ya Ujerumani ambayo Marekani ilichangia mno.....Katika hotuba yake, bibi Angela Merkel, alifungamanisha tena na tena hatima yake binafsi na ya nchi yake.Akakumbusha jukumu la Ujerumani katika madhila ya vita vya pili vya dunia.Lakini pia, kuzigirwa kwa jiji la Berlin na ujenzi wa ukuta.

Kutokana na maarifa yake binafsi aliopata,Kanzela Merkel , aliusimulia ukumbi kuanguka kwa ukuta na kuishi nyuma ya uwa wa senyenge ,kukiwaathiri vipi wakaazi kama yeye wa iliokua Ujerumani Mashariki.Alishangiriwa mno kwa kupigiwa makofi pale alipotoa shukurani zake kwa Marekani kwa kupigania uhuru wa ile sehemu moja ya Ujerumani:

"Naelewa na sisi wajerumani tunaelewa kiasi gani tutoe shukurani zetu kwa marafiki zetu wamarekani.Kamwe, hatutasahau,kamwe, mimi binafsi sitawasahau."

Bibi Merkel ambae kabla hotuba yake alikutana na rais barack Obama ,alisisitiza usuhuba mkubwa uliopo kati ya Ujerumani,Ulaya na Marekani ambao hauegemei tu masilahi ya pamoja ,bali hasa desturi za maadili ya pamoja.

Akaongeza,

"Amerika na ulaya kusema kweli , sio daima zina maoni sawa.Upande mmoja baadhi ya wakati, ukimuona mwenzake anasitasita kuamua na akionesha woga; na mwengine, akimuona mwenziwe anajiamulia atakavyo na kuwashinikiza wenzake.Juu ya hivyo:Ninaamini kabisa , mshirika bora kuliko Marekani hakuna.Na mshirika bora kwa Marekani, kuliko ulaya, hayupo."

Katika hotuba yake kwenye Bunge hilo la Marekani, Kanzela Merkel, aligusia pia mada nyengine: Aliungamkono mchango wa Ujerumani inaotoa nchini Afghanistan na kusema kwamba, Ujerumani haitarudi nyuma katika jukumu lake ililojitwika huko.Alisisitiza pia umuhimu inaouambatisha Ujerumani katika kundi la nchi tajiri la G-20 katika kutunga mfumo wa masoko ya fedha ulimwenguni.Akahimiza kuwapo sera- endelevu ya kuufufua uchumi ulimwenguni.

Merkel, alisisitiza haki ya kuwapo kwa dola la Israel; na akatangaza kwamba ataungamkono utaratibu wa amani katika Mashariki ya Kati wenye shabaha ya suluhisho la dola 2.

Kuhusu ugomvi juu ya mradi wa kinuklia na Iran, Kanzela Merkel, alisema ,

"Bomu la atomiki mikononi mwa rais wa Iran anaekanusha msiba wa kuhilikishwa wayahudi-Holocaust,anaeitishia Israel na kuwapo kwa dola la Israel,halifai kuwapo."

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Uhariri: Abdul-Rah