1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karachi: Maandamano kupinga shambulio lilo mlenga Bhutto yaendelea.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ds

Mamia ya waandamanaji katika mji wa kusini mwa Pakistan-Karachi, wamechoma moto matairi ya magari na kurusha mawe leo, ikiwa ni siku ya tatu mfululizo kupinga shambulio dhidi ya msafara wa waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto ambapo watu 139 waliuwawa. Maandamano ya upinzani sawa na hayo yamefanyika pia katika miji ya Hyderabad, Nawabshah, Sukkur na wilaya walikotoka wahanga wa hujuma hizo za mabomu, zilizotokea muda mfupi baada ya Bibi Bhutto kurudi nyumbani kutoka uhamishoni alikoishi kwa miaka minane. Wakati huo huo akizungumzia uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kati kati ya Januari mwakani, Waziri mkuu Shaukat Aziz alisema, haoni utaratibu wa uchaguzi ukiathirika, lakini bila shaka wanapaswa kuwa na busara na pengine kulazimika kubadili mikakati kidogo.