1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karachi. Mvua zaua watu kadha.

25 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBog

Baadhi ya sehemu za kusini mwa Asia zimekumbwa na dhoruba na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko. Zaidi ya watu 220 wamepoteza maisha katika matukio yaliyosababishwa na mvua pamoja na upepo mkali kusini mwa Pakistan, kiasi kikubwa ikiwa ni katika mji wa bandari wa Karachi.

Wengi wa waliouwawa ilikuwa ni kutokana na kunaswa na umeme wakati majengo pamoja na nguzo za umeme zikianguka.

Kusini magharibi ya India , kiasi watu 45 wameuwawa kutokana na mvua kubwa pamoja na radi, ambapo maelfu kadha ya watu wameachwa wakiwa hawana makaazi.