1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KARACHI: Shambulizi limeua mamia ya watu Pakistan

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ea

Watu wasiopungua 126 wameuawa nchini Pakistan, katika shambulizi la bomu lililomlenga waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo,Benazir Bhutto.Si chini wa 260 pia wamejeruhiwa.Miripuko miwili ilitokea karibu na basi ambamo Bhutto alikuwepo lakini hakujeruhiwa.Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo,lakini wanamgambo wanaowaunga mkono Wataliban,walionya kuwa watamuua Bhutto atakapowasili.Benazir Bhutto amerejea nyumbani baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka minane na anataka kugombea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanywa mwezi wa Januari.

Umoja wa Ulaya na Marekani zimelaani mashambulizi hayo.Rais Pervez Musharraf wa Pakistan pia amesema,mashambulio hayo ni njama dhidi ya udemokrasia.