1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karachi. Waziri ajeruhiwa kwa bomu.

29 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC64

Kiasi watu 26 wameuwawa na wengine kadha wamejeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga nchini Pakistan. Miongoni mwa waliojeruhiwa ni pamoja na waziri wa mambo ya ndani Aftab Khan Sherpao, ambaye anasemekana kuwa alikuwa mlengwa wa shambulio hilo.

Sherpao alikuwa amemaliza hotuba yake katika mji wa Charsada ulioko katika jimbo la mpakani la kaskazini magharibi wakati mshambuliaji huyo wa kujitoa muhanga alipofyatua milipuko hiyo. Mmoja kati ya wasaidizi wa waziri huyo na wengi miongoni mwa walinzi wake wameuwawa katika shambulio hilo.