1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KARACHI:Benazir Bhutto akaribishwa kwa shangwe

18 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Eg

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto amerejea nchini humo baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka minane.

Bibi Bhutto aliwasili aliwasili mjini Karachi mchana leo kutoka Dubai

Bibi Bhutto amerejea nchini Pakistan kukiongoza chama chake cha Pakistan Peoples Party.

Takriban wafuasi laki mbili na nusu wamekusanyika mjini Karachi kumlaki waziri huyo mkuu wa zamani.

Msemaji wa chama cha Pakistan Peoples Party Bibi Sherrry Rehman amesema.

Benazir Bhutto alikabiliwa na mashtaka ya rushwa wakati alipoondoka nchini Pakistan muda mfupi baada ya rais Pervez Musharraf alipochukuwa madaraka mwaka 1999.

Rais Musharraf amemuondolea mashtaka hayo bibi Bhutto lakini mahakama kuu inasubiriwa kuamua iwapo msamaha huo una ambatana na sheria.

Usalama umeimarishwa kufuatia vitisho vya makundi ya Al Qaeda na Taliban kwamba watamuua bibi Benazir Bhutto.