1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KARACHI:Benazir Bhutto amerejea nchini Pakistan

18 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Eo

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan bibi Benazir Bhutto amewasili mjini Karachi.

Bibi Bhutto amerejea nchini Pakistan kukiongoza chama chake cha Pakistan Peoples Party baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka minane.

Maelfu ya wafuasi wake walikusanyika katika uwanja wa ndege wa mjini Karachi kwa ajili ya kumlaki.

Bibi Benazir Bhutto alikabiliwa na mashtaka ya rushwa wakati alipoondoka kutoka nchini Pakistan mara tu rais Pervez Musharaf alipochukuwa madaraka mwaka 1999.

Rais Musharraf amemuondolea mashtaka hayo bibi Benazir Bhutto lakini mahakama kuu nchini Pakistan inasubiriwa kuamua iwapo msamaha huo unaambatana na sheria.

Hali ya usalama imeimarishwa kufuatia vitisho vya makundi ya Al Qaeda na Taliban kwamba watamuua bibi Benazir Bhutto.