1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KARACHI:Musharraf amuonya Bush

8 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBb9

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan ameionya Marekani kuanzisha mashambulizi dhidi ya kundi la kigaidi la Al Qaida katika ardhi yake.

Musharraf alimwambia Seneta Richard Durbin wa Marekani aliyeko ziarani nchini humo, kuwa kuzungumza juu ya uwezekano wa Marekani kuwashambulia Al qaida waliyoko Pakistan hakuna faida yoyote.

Amesema kuwa ni majeshi ya nchi yake tu ndiyo yatakayobeba dhamana ya kupambana na ugaidi ndani ya ardhi yake.

Kauli hiyo ya Musharraf inakuja siku moja babada ya Rais George Bush kusema kuwa jeshi la Marekani linaweza kupepeleza na kuwashambulia viongozi wa Al qaida ndani ya Pakistan.Hata hivyo Rais Bush hakusema kama Pakistan itashauriwa mapema kabla ya hatua hiyo.