1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KARBELA :watu wengine 58 waangamia nchini Irak

29 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC5z

Watu wasiopungua 58 wameuawa katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji wa Karbala nchini Irak.

Shambulio hilo lilifanyika kwenye kitongoji muhimu cha biashara karibu na sehemu takatifu ya washia. Watu wangine wapatao 170 walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Wakati huo huo askari wengine 9 wa Marekani wameuawa.Taarifa iliyotolewa na jeshi la Marekani imefahamisha kwamba askari wanne kati ya hao waliuawa kutokana na mabomu yaliyotegwa njiani na wengine watano waliuliwa katika mapambano na wapinzani .

Habari zaidi kutoka Irak zinasema wapinzani 72 wamekamatwa na majeshi ya Marekani mapema asubuhi leo katika jimbo la Anbar magharibi ya Baghdad.

Wengine walikamatwa katika jimbo la Salahuddin maili 60 kaskazini ya mji mkuu. Watu hao wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida.