1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karibu watu alfu kumi watafukuzwa kazi kutoka kampuni ya Ulaya ya kutengene ndege , Airbus

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCNj

Kampuni ya kutengenza ndege hapa Ulaya, Airbus, imehakikisha kwamba inapanga kuviuza viwanda vyake viwili na kupunguza uzalishaji katika vingine vinne. Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Louis Gallois, ataufichua baadae leo mpango wa kuifanyia marekebisho kampuni hiyo utakaogharimu Euro bilioni tano. Vyama vya wafanya kazi katika Ufaransa vimesema maafisa wa kampuni hiyo ya Airbus wamehakikisha nafasi za kazi alfu kumi zitapunguzwa, nusu kati ya hizo ziko katika kampuni zinazopewa kandarasi. Kampuni hiyo imesema viwanda vilioko Nordenham hapa Ujerumani, Meaulte na Saint-Nazaire-Ville huko Ufaransa pamoja na kile cha Filton nchini Uengereza vitaathirika kutokana na mpango huo wa marekebisho. Mjini Brussels, maafisa wa vyama vya wafanya kazi kutoka Uengereza, Ufaransa, Ujerumani na Spain wamekutana kuowanisha mikakati yao.

Katibu mkuu wa vyama vya wafanya kazi wa viwanda vya vyuma katika Ulaya, Peter Sherrer, amesema:

+Sisi tuko tayari kutafuta suluhisho na tuko tayari kufanya mazungumzo, lakini ikiwa mambo yatajitokeza kama vile tulivohofia, basi hapo tutajikusanya na kujipanga, na matokeo yake ni kwamba katika baadhi ya sekta kutakuweko migomo.+