1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KARLSRUHE: Mahakama ya Rufaa yakataa kusikiliza rufani ya kesi ya mshukiwa wa ugaidi.

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC32

Mahakama ya mwisho ya rufaa ya Ujerumani imekataa kusikiliza rufani dhidi ya hukumu ya kesi ya raia wa Moroko aliyepatikana na hatia ya kuwasaidia marubani watatu miongoni mwa marubani kumi na mmoja waliohusika katika mashambulio ya Septemba tarehe kumi na moja nchini Marekani.

Mahakama hiyo iliyoko Karlsruhe ilitoa taarifa ikisema rufani ya kesi ya Mounir al-Moutassadeq haina uzito wowote.

Uamuzi huu una maana kwamba Mounir al-Moutassadeq hana budi ila kutumikia kifungo cha miaka kumi na mitano gerezani alichohukumiwa.

Mounir, mwenye umri wa miaka thelathini na mitatu, mwezi Novemba mwaka uliopita alipatikana na hatia ya kuwasaidia waliohusika na mauaji ya abiria mia mbili na arobaini na sita pamoja na wahudumu wa ndege nne zilizotumiwa katika mashambulio hayo ya mwaka 2001 nchini Marekani.