1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karlsruhe, Ujerumani. Mahakama yaruhusu upelekaji wa Tonado Afghanistan.

13 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJf

Mahakama ya katiba nchini Ujerumani iliyoko katika mji wa Karlsruhe imeondoa kikwazo cha mwisho kilichokuwa kinazuwia upelekaji wa ndege sita za upelelezi chapa Tonado pamoja na wanajeshi wengine 500 nchini Afghanistan.

Jopo la majaji lilitupilia mbali maombi ya kuzuwia upelekaji wa ndege hizo, ambayo yametolewa na wabunge wa wawili wa baraza la wawakilishi katika bunge la Ujerumani.

Bunge la Ujerumani Bundestag liliidhinisha upelekaji wa ndege hizo Ijumaa iliyopita. Ndege hizo za Tonado zitatumika kuangalia maeneo muhimu ya kushambulia kwa ajili ya jeshi la NATO pamoja na majeshi yanayoongozwa na Marekani.

Ujerumani tayari ina kiasi cha wanajeshi 3,000 walioko kaskazini ya Afghanistan.