1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karzai azungumzia amani

5 Septemba 2010

Baraza jipya la amani Afghanistan liko tayari kwa mazungumzo na taliban.

https://p.dw.com/p/P4Z2
Rais Hamid Karzai wa AfghanistanPicha: AP

Rais Hamid Karzai amesema baraza jipya la amani la nchi hiyo, lililoundwa kwa minajili ya kuwanyooshea mkono wataliban, liko tayari kwa mazungumzo na kundi hilo. Lakini hadi sasa Kundi la Taliban limepuuza juhudi hizo za serikali, likisisitiza kwanza lazima vikosi vyote vya kigeni viondoke Afghanistan. Chini ya mpango huo wa Karzai, watakaoasi kundi la Taliban watakirimiwa kwa fedha na nafasi za ajira. Nao viongozi wa ngazi ya juu wa Taliban watatafutiwa hifadhi katika nchi za Kiislamu. Mpango huo wa Karzai unawiana na pendekezo la Marekani na washirika wake wa NATO, ambao wana wanajeshi laki moja na nusu Afghanistan, kuwapa jukumu la usalama wa nchi yao wanajeshi wa Kiafghani. Wakati huo huo, bomu lililokuwa limetegwa katika honda liliripuka katika mji wa Kaskazini wa Kunduz na kuwaua raia wanne na maafisa watatu wa polisi. Na katika mji wa kusini wa Kandahar mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliwaua watu watatu wakati alipojaribu kuuripua msafara wa magari ya wanajeshi wa Jumuiya ya kujihami ya NATO.