1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kashfa katika Kanisa Katholiki Ujerumani

23 Februari 2010

Visa zaidi vya vichuliwa vya kuharibiwa watoto.

https://p.dw.com/p/M90i

Visa mia kadhaa vya kuharibiwa watoto wadogo katika Taasisi za Kanisa Katoliki nchini Ujerumani ,hivi sasa vimefichuliwa.Kila kukicha, wahanga wapya wanajitokeza na kusimulia yaliowafika.Kashfa hii awali iliibuka hadharani katika Shule ya makasisi ya Jesuite mjini Berlin.

Mwanzoni kabisa , kashfa hii ya kuharibiwa watoto, ilianzia shule ya (Canisius-Kolleg ) kutokana na makala iliochapishwa katika kigazeti cha makasisi wa (Jesuite )Desemba mwaka uliopita.Ursula Raue,mjumbe wa kundi hilo la makasisi anaeshughulikia visa vya kuharibiwa watoto alitoa nasaha ndani ya gazeti hilo vipi wazee wa watoto hao na walimu wao, wakabiliane na visa vya uharibifu vinavyosemekana kutendeka.

Bibi Raue alieleza:

"Makala yangu ilichukuliwa na Padri Pater Mertes na akawapelekea wazee wote wa wanafunzi wa shule ya Canisius.Hii yadhihirika, ilizusha mjadala moto-moto mjini Berlin.Watu kadhaa wakaripoti na kusema kwamba,hata siku za nyuma nao, yaliwafika mambo kama hayo wakati walipokuwa katika shule hii. "

Hadi Januari, mwaka huu, walijitokeza wahanga 7 kwa mkuu wa shule hiyo ya -Canisius Kolleg ,Padri Klaus Mertes.Mertes ambae tangu 1994 anafanya kazi katika shule hiyo ,alianza kukusanya visa hivyo vilivyoripotiwa kwake na kuwaandikia barua wanafunzi wa zamani wa shule hiyo.Katika barua hizo aliomba radhi kwa waliofikwa na maafa hayo kwa niaba ya shule hiyo. Katika chumba cha mkuu wa shule hiyo , simu ikilia mfululizo.Pater Klaus Mertes, akawa anajibu maswali ya waandishi habari.

"Kwa muujibu wa sheria, mashtaka ya kuwaharibu watoto wadogo ,muda wake wa kushtaki hupita baada ya miaka 10 na baada ya mhanga kufikia umri wa miaka 18.Kwahivyo, visa hivi, haviwezi sasa kufikishwa mahkamani.Kile tuwezacho kufanya, ni kumpa jukumu mjumbe wetu anaeshughulikia visa hivi, kukabiliana na waliofanya madhambi hayo na kufanya utafiti ili kujua kilipita nini na kusimama pamoja na wahanga."

Mkasa huu, ni wa kwanza kwa Taasisi ya kanisa katholiki humu nchini kuuripoti hadharani.Stefan Dartmann, ni Kiongozi wa madhehebu hiyo nchini Ujerumani.Anasema kwamba, wahanga wa uharibifu huo wanateseka na ukumbusho wa vitendo vilivyowafika na sasa wanapaza sauti zao Ana washukuru kwa kufanya hivyo na kuwaomba maradhi kwa waliotendewa wakati wakiwa katika shule hiyo ya Jesuite.Pia anaomba radhi kwa wale wakati ule waliokuwa na dhamana shuleni na kuyafumbia macho madhambi hayo.

Baada ya kwanza kupata sifa kwa shule hii ya Jesuite kwa kuanika hadharani maovu yaliotendeka ,baadae ilikosolewa.Kwani, Padri Mertes aliungama kwamba, wahanga waliripoti kwake visa vilivyowapata tayari miaka 5 nyuma.Hakufichua hayo hadharani kwavile, alisema kuwa, aliwahakikishia waliompa taarifa hizo kwamba, angeziweka siri.Wakuu wenye dhamana katika Taasisi hiyo, walikwishajua juu ya tuhuma hizo muda mrefu kabla .

Kwani, mmoja kati ya waliofikwa na maafa hayo, aliripoti gazetini kwamba, mama yake alimkabili mkuu wa zamani wa shule hapo 1975 juu ya kisa cha kuharibiwa mwanawe. Ilibainika pia kwamba, walimu waliolaumiwa kuwaharibu watoto , wakihamishiwa shule nyengine.

Kwa jumla, hata shule nyengine za (Jesuite) nchini Ujerumani, zimeripoti nazo mikasa kama hiyo ya kuharibiwa watoto wadogo.

Mwandishi: Bölinger,Mathias

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed