1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kashfa za Ulawiti Ireland zaliandama Kanisa Katoliki

15 Februari 2010

Papa Benedikti XVI awaita Maaskofu wa Ireland,Vatikani.

https://p.dw.com/p/M1q2
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedikti XVIPicha: AP

Kashfa ya vitendo vya ulawiti inayowaandama mapadiri nchini Ireland pamoja na kufichwa kwa visa hivyo, ni changamoto kubwa hii leo katika mkutano aliuitisha kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Benedikti wa kumi na sita amewaita maaskofu wote wa Kikatoliki nchini Ireland kukutana naye katika makao makuu ya Kanisa hiyo huko Vatikan kuzungumzia kashfa hiyo. Mohamed Abdul-Rahman anayo zaidi

Kashfa hiyo ilioikumba Ireland ambayo asili mia kubwa ya wakaazi wake ni wa madhehebu ya Kikatoliki, ilizuka mwezi Novemba kwa kuchapishwa ripoti mbili za kisheria kuhusiana na vitendo vilivyofanywa na mapadiri-ripoti iliozusha mshtuko mkubwa. Padiri mmoja alikiri kuwalawiti zaidi ya watoto 100 ambapo mwengimne alikiri kwamba alikuwa akiwalawiti wavulana wadogo kila baada ya wiki mbili kwa muda wa miaka 25.

Makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani yana wasi wasi kwamba vitendo hivyo ambavyo ni wimbi la hatari, vinaweza vikasababisha waumini wengi kulihama kanisa hilo na hata kupoteza kabisa imani na kuwakatisha tamaa.

Mwezi Januari mwaka huu mgogoro huo nchini Ireland ulifuatiwa na kashfa nchini Ujerumani, wakati mhubiri mmoja kutoka shule ya Kristo mjini Berlin alipokiri kwamba walimu waliwalawiti vijana mnamo miaka ya 1970 na 80. Vatikani ilisema Papa Benedikti wa 16 anapanga kutoa barua ya Kanisa kwa Wakatoliki nchini Ireland kuhusu Kashfa hiyo, ikiwa na lengo la kurudisha imani na njia madhubuti za kuepusha vitendo vya aina hiyo miongoni mwa mapadiri ndani ya Kanisa.

Hata hivyo mwanaharakati mmoja ,mpinzani wa visa vya unyayasaji amemtaka Papa Benedikti wa 16 aizuru Ireland na kukutana binafsi na wahanga wa vitendo hivyo vya ulawiti, kama alivyofanya huko Australia na Marekani. Bibi Christine Buckley ambaye binafsi ni mhanga wa visa vya unyanyasaji akaongeza kwamba Kiongozi huyo mkuu wa kanisa Katoliki duniani anapaswa kuwaomba radhi wahanga kwa niaba ya Kanisa.

Tayari Papa Benedikti anayeliongoza Kanisa hilo lenye waumini bilioni 1.1 duniani. alikutana na Viongozi wawili wa ngazi ya juu wa kanisa nchini Ireland Kadinali Sean Brady na Askofu mkuu wa Durblin Diarmuid Martin na baadae akasema anaungana na waumini walikumbwa na aibu na kusalitiwa, kama wanavyohisi wengi miongoni mwa waumini nchini Ireland.

Mwandishi:Abdul-Rahman,Mohammed/Reuters

Mhariri:Thelma Mwadzaya.