1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KATHMANDU: Duru mpya ya mazungumzo ya amani

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4w

Nchini Nepal,serikali na waasi wa kikomunisti wamerejea tena kwenye majadiliano yao ya amani.Waziri mkuu Giriya Prasad Koirala amekutana na kiongozi wa waasi Prashand mjini Kathmandu.Majadiliano hayo hasa yanashughulika na suala la kuwanyanganya silaha waasi na vile vile mustakabali wa ufalme nchini humo.Serikali inawataka wakomunisti watoe silaha zao,kabla ya kushiriki katika serikali ya mpito iliyokubaliwa tangu mwezi wa Juni.Serikali hiyo inatazamiwa kutayarisha katiba mpya ya nchi.Majadiliano ya amani kati ya pande hizo mbili yalivunjika kati kati ya mwezi Juni.