1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KATHMANDU: Makundi mawili yadai kuhusika na mashambulio ya mabomu

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBT3

Makundi mawili kutoka eneo la Terai kusini mwa Nepal, leo yamedai kuhusika na mashambulio ya mabomu yaliyosabaisha vifo vya watu wawili mjini Kathmandu nchini Nepal.

Mabomu hayo yaliyolipuka karibu wakati mmoja yalizusha hasira miongoni mwa viongozi wa serikali, waasi wa zamani wa Mao na Umoja wa Mataifa. Watu zaidi ya 20 walijeruhiwa kwenye milipuko hiyo.

Mashambulio hayo yamemaliza kipindi cha utulivu na amani katika bonde la Kathmandu kilichoanza baada ya waasi wa Mao na serikali kufikia makubaliano ya amani mnamo mwaka jana. Makubaliano hayo yalimaliza upinzani uliosababisha vifo vya watu takriban 13,000 nchini Nepal.

Wakati haya yakiarifiwa, polisi nchini Nepal hii leo wameanza uchunguzi huku wakiyasaka magari na wapita njia mjini Kathmandu.