1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KATHMANDU:Wanaharakati wakimao na wafuasi wao waandamano dhidi ya utawala wa kifalme

30 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLJ

Maelfu ya wananchi wanaounga mkono wanaharakati wakimao nchini Nepal wameandamana katika mji wa Kathmandu hii leo kuanza kampeini ya kulazimisha mageuzi katika taifa hilo ikiwa ni pamoja na kutaka kuondolewa kwa utawala wa kifalme.

Wanaharakati wakimao waliosaini makubaliano ya amani na vyama vya kisiasa nchini humo mwezi Novemba waliingilia serikali kiasi wiki mbili zilizopita wakilalamika kwamba hawatendewi sawa kama washirika serikalini.Kundi la wanaharakari wakimao walioingia serikalini pia walidai kwamba mfalme Gyanendra aliyepoteza umaarufu wake pamoja na wafuasi wake jeshini wanapanga kufanya mapinduzi yenye lengo la kuzuia hatua za kuuondoa utawala wa kifalme.Hatma ya utawala wa kifalme nchini Nepal imepangwa kuamuliwa baada ya uchaguzi mwezi Novemba 22 lakini mrengo wa shoto unataka utawala huo uondolewe mara moja na pia pafanyike mageuzi ya uchaguzi na Nepali itangazwe kuwa nchi ya jamhuri kabla ya kipindi cha uchaguzi.