1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katumbi aibua muungano vyama tawala Kongo

Jean- Noel19 Desemba 2022

Baada ya kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Moses Katumbi, kutangaza rasmi kuwania urais 2023, muungano wa vyama vilivyo madarakani wawataka raia kutochagua mgombea mwenye uraia wenye mashaka.

https://p.dw.com/p/4L9la
Demokratische Republik Kongo I Staatspräsident Félix Tshisekedi in Kinshasa
Picha: Giscard Kusema/Präsidialamt Kongo

 Kupitia tangazo lake la kugombea urais, gavana huyo wa zamani wa mkoa wa Katanga ambaye ni kiongozi wa chama Ensemble pour la République alihakikisha kujiondoa kwake katika muungano wa vyama vinavyomuunga mkono Rais Félix Tshisekedi.

Muungano wa vyama tawala unaodai kuunga mkono demokrasia hapa nchini Kongo umeeleza kuwa hauwezi kutishwa na ugombea wa Moses Katumbi, ila sharti akidhi vigezo vilivyowekwa na sheria ya uchaguzi pamoja na katiba ya nchi hii.

Kwa mjibu wa Thierry Monsenepo, mmoja wa viongozi wamuungano huo, Rais Félix Tshisekediameutumia muhula wake wa kwanza ipasavyo kwa kutekeleza aliyoyaahidi na sasa anataka kuendelea kuhudumu tena kwa muhula wa pili.

Soma zaidi:Moise Katumbi amtambua Felix Tshisekedi kama rais wa DRC

 Monsenepo amewataka Wakongo kuchagua kati yake na Moses Katumbi ambaye uraia wake unabaki wa mashaka na Tshisekedi.

"Kumbukeni kuna wakati Katumbi alijitokeza mbele ya hadhara ya raia wa Kiyahudi akiwaeleza kuwa yeye anachukiliwa hapa Kongo kwani yeye ni mtoto wao."

Amesema hayo huku akirejea asili yamwanasiasa huyo na kuongeza kwamba  baba wa mwanasiasa huyo ni ni Mtaliano wa  asili ya Kiyahudi na mama yake  ni Mzambia.

"Hana uhusiano wowote kuhusu uraia wa Kongo kufuatana na yale yanayoelezwa na Katiba ili kudai kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri."

Sio mara kwanza kushutumiwa kuhusu uraia

Utawala wa rais wa zamani, Joseph Kabila, uliwahi kumshutumu Katumbikuwa siye raia wa Kongo na hivyo ukamnyang'anya paspoti yake.

Lakini alipoingia madarakani, Rais Tshisekedi alimrejeshea pasipoti hiyo na hivyo kuthibitisha kwamba Katumbi ni raia wa Kongo. Kinachoshangaza ni kuona leo utawala huo huo ndio unaeleza kama Katumbi ni mgeni.

DRC Afrika Treffen Moise Katumbi
Mwanasiasa nchini Kongo Moise KatumbiPicha: presidential press service of the DRC

Wachambuzi wa mambo wanasema Katumbi ndiye mwanasiasa anayeonekana kuwa tishio kubwa dhidi ya Tshisekedi kwenye uchaguzi ujao na hivyo kubabaisha sana chama kilicho madarakani.

Licha ya Katumbi kuwa mshirika katika muungano wa Tshisekedi, wawili hao waliishi kwa mashaka makubwa na kutoaminiana kipindi chote cha kuwamo kwenye muungano huo.

Hatua ya kujiondoa kwake kutoka muungano huo kulikuwa kumetarajiwa, na wafuatiliaji wa siasa za nchini humo kutokana na mienendo ya mwanasiasa huyo.

Soma zaidi:Mazungumzo ya Rais Tshisekedi na wapinzani yakwama

 Anselme Kyungu, mhadhiri  katika Chuo Kikuu cha Kolwezi mkoani Lualaba ameambia DW Kiswahili kwamba hilo si  jambo la kushangaza kwani Moses hajawahi kuwa mshirika wa Tshisekedi isipokuwa tu kwa maslahi.

"Wengi wa wanachama wake walieleza kwamba hawawezi kufanya siasa bila kuchukuwa madaraka. Yaani wengi wako katika muungano wa rais pia serikalini kwa maslahi yao tu. Unajua mara nyingi kulikuwa na jaribio la kujitenga."

Jina la Moses Katumbi hivi sasa limeongezwa kwenye orodha ya wagombea ambaotayari wamejitangaza rasmi kupambanana Rais Félix Tshisekedi hapo mwakani.

Wengine ni mawaziri wakuu wa zamani, Augustin Matata na Adolphe Muzito, pamoja na viongozi wengine wa upinzani, akiwemo Martin Fayulu, Justin Mudekereza na Jean-Marc Kabund. Uchaguzi unatarajiwa kufanyika tarehe 20 Desemba 2023.