1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenenisa Bekele aipatiia Ethiiopia medali ya dhahabu

18 Agosti 2009

Shelly-Ann Fraser-dhahabu kwa Jamaica

https://p.dw.com/p/JDRX
Kenenisa Bekele (Ethiopia)Picha: AP

Katiika siku ya tatu ya mashindano ya riadha ulimwengunii mjini Berlin,Muethiopia Kenenisa Bekele alimuigiza bingwa wake Haile Gebrselassie kwa kushinda kwa mara ya 4 mfululizo tajii la mita 10.000 akizima vishindo vya waeritrea na wakenya.Shelly-Ann Fraser wa Jamaica, alifyatuka nae kama kombora na kumpiiku mwenzake Kerron Stewart na kuipatiaJamaica taji lake la piili la mita 100 baada ya lile la siku moja kabla la Usain Bolt.

Haikua siku njema kwa wanariadha wa Ujerumanii,kwani jana walitoka mikono mitupu.Msichana wa Kenya Milcah Chemos Cheywa,lakini anarudii Nairobi na medalii ya shaba katika mbio za mta 3000 kuruka viunz ambazo jioni ya leo wenzake wakiume waahidi kuongeza nyengine 3-dhahabu,fedha na shaba.

Kenenisa Bekele hakuchelewa kutia fora usonii mara kengele ya duru ya mwisho ilipolia na mwishoe, alishinda tajii lake la 4 la dunia kwa muda wa rekodi ya mashindano haya wa dakika 26:45.31.Kwa ushindi huo,Bekele ameseleleza rekodi yake ya kutoshindwa katika mashindano yote 4 ya mita 10.000 pamoja na mataji yake 2 ya olimpik.Zersenay Tadese wa Eritrea alieongoza mbio hizo tangu mwanzo, alishinda medali ya fedha huku Moses Masai wa Kenya, akibidi kuridhika na medali ya shaba kuongezea ile ya dhahabu ya dada yake Linet Masai aliewapokonya waethiopia Jumamosii.

Maajabu yalzuka katika mita 3000 kuruka viunzi,kwani mhispania Dominiquez altimka mbiio na kumpita mrusi Yuliiya Zarudneva kunyakua medal ya dhahabu.Bngwa wa Olimpiik Gulnara Galkina almalza 4 nyuma ya mkenya Chemos Cheywa aliondoka na medal ya shaba.

Kulizuka msangao katka nusu-finali ya mbio za mita 800 wanawake: Biingwa wa olmpk kutoka Kenya pamela Jelimo alijitoa nje ya mbio hizo na sasa hana nafasi katika finali .Mwenzake kutoka Kenya,bingwa wa duna Jeneth Jepkosgei aliinga chupuchupu tu finali ya hapo kesho.Mzaliwa wa kenya anaekimbia kwa Marekani katika mita 1500 Bernard Lagat amekata tikleti ya finali ya kesho ya mbiio hizo akikaa tayar kupambana na mkenya Abel Kirop.

Maajabu yalizuka katika mashindano ya Pole vault-kuruka juu kwa upongoo: Malka wa mashindano hayo Yelena Isinbayeva wa Russia, alshindwa hata kukiuka kipimo cha kwsanza cha mita 4.75.Taj llikwenda kwa mpoland Anna Rogowska.Msichana wa Ujerumani ,Silke Spiegelburg alikosa medali ya shaba chupuchupu kwa kushindwa kuruka mita 4.75 cm.

"Knachonsiktisha sana nilikiona kipimo cha mita 4.75 niliporuka mara ya kwanza,lakini nilishndwa na kuangusha na sasa mnimetokea 4. iilhali niingeweza kuondoka na medali."Usiku wa leo huenda ukawa wa wakenya katika miita 3000 kuruka viunzi:

Muandshi: Ramadhan Ali

Mharir: Mohammed Abdul-Rahman