1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya : Bila nishati hakuna maendeleo

18 Agosti 2008

Mwenyekiti wa uratibu wa umeme ERC nchini Kenya asema kuwa hakuna uhaba wa umeme nchini Kenya.

https://p.dw.com/p/Ez9Q

Kwa kawaida busara inaonyesha kuwa upungufu wa nishati rahisi na ya kutegemewa ni kipengee muhimu katika kuimarisha maendeleo katika ngazi ya chini katika nchi kama Kenya.

Lakini mratibu mkuu wa masuala ya nishati nchini humo anadai kuwa Kenya ina nishati ya kutosha inayoihitaji, na ongezeko la nishati hiyo halipaswi kupita ukuaji wa mahitaji ya nishati.

Iwapo utaniuliza kama upo uhaba wa umeme nchini Kenya, naweza kusema upo na pia haupo, anasema hivyo Hindpal Singh Jabbal , mwenyekiti wa tume ya kuratibu nishati ERC nchini Kenya.

Tunakaribia kufikia mahitaji yetu ya hivi sasa ya umeme. Hakuna tatizo la kukatika kwa umeme, na hakuna tatizo la matumizi makubwa. Mwanya baina ya mahitaji na upatikanaji ni mdogo sana.

Lakini kwa upande wa fedha na gharama ya uzalishaji wa umeme, sio tu nchini Kenya lakini hata Tanzania na Uganda zinakumbana na matatizo ya kukatika kwa umeme, amesema mkuu huyo wa tume ya uratibu wa nishati nchini Kenya. Jabbal anaona utegemezi wa kushuka kwa uwezo wa vinu vinavyotumia nguvu ya maji kufua umeme kuwa moja ya sababu zinazokwaza uzalishaji wa umeme.

Miaka michache iliyopita, asilimia 80 ya nishati nchini Kenya ilikuwa inapatikana kutokana na vyanzo vya nguvu za maji. Mgao huo sasa uko chini ya asilimia 45, ambapo vyanzo vingine vya nishati kama jua na upepo vinatoa asilimia 15 na vinu vinavyotumia aina moja ama nyingine ya mafuta ya petroli ikiwa ni asilimia 40.

Mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa asilimia saba kila mwaka, licha ya kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watu wanaoishi vijijini hawana umeme. Katika muda wa miaka mine ijayo, Jabbal anasema , Kenya itaachana na vinu vinavyotoa nishati ghali ya dharura, vinu vya dharura vya nishati vinavyotumia mafuta ya diseli na vinu vinavyoendeshwa kwa gesi vikitumia mafuta ya taa na kutegemea zaidi mashine zinazotumia mafuta mazito na vyanzo vingine vya nishati endelevu vinatoa megawati za ziada 70 hadi 80 zinazohitajika kila mwaka.

Nishati mbadala ndio zinazotarajiwa kutumika katika wakati ujao, amedokeza Jabbal. Hatuna mkaa wa mawe hadi sasa , hatuna gesi ama mafuta. Bonde la ufa linautajiri mkubwa wa nishati mbadala na nishati kwa kiasi kikubwa ya nchi hii itatoka katika chanzo hiki.

Amekiri kuwa kuna athari mbaya za mazingira kwa kutumia vyanzo hivi, lakini ameongeza kuwa hali hiyo itaondolewa kutokana na ukweli kuwa nishati hiyo mbadala haina gesi ya Carbon. Athari yake kubwa kwa kilimo inafahamika , lakini kwa bahati, vinu vya nishati hiyo nchini Kenya vitawekwa katika maeneo kame ya bonde hilo ambako hakuna shughuli za kilimo.Hatufahamu kwa ukamilifu uwezo wa vyanzo vya nishati ya jua na upepo. Inaweza kuwa kati ya megawati 2000 hadi 7,000. Lakini ni hatua kubwa mbele. Si wataalamu wote wa nishati wanakubali mawazo ya Jabbal. Wengi wao wanaamini kuwa ukuaji wa kiuchumi unategemea sana upatikana wa kutosha wa nishati na Kenya inamatatizo katika hilo.