1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Chama Cha CORD kuwasilisha malalamiko Mahakamani

14 Machi 2013

Nchini Kenya,muungano wa CORD unaoongozwa na Raila Odinga uko tayari kuwasilisha malalamiko yake katika mahakama ya juu hapo kesho kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi wa machi 4.

https://p.dw.com/p/17xCN
Waziri Mkuu Raila Odinga
Waziri Mkuu Raila OdingaPicha: Getty Images/AFP

Kulingana na mmoja wa mawakili wa Muungano huo Eliud Owalo Cord imo mbioni kutafuta haki ya wa kenya ili wapate kuongozwa na Rais waliomchagua. Cord inadai uchaguzi mzima ulioandaliwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya ulikuwa na hitilafu nyingi.

Muda mfupi uliopita Amina Abubakar alizungumza na wakili Eliud Owalo na kwanza anaelezea wamefikia wapi kwa sasa katika hatua yao ya kuwasilisha kesi hiyo. Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman