1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Tishio la mashambulizi ya kigaidi mjini Mombasa

16 Mei 2014

Nchini Kenya , Wakala mmoja wa usafiri lwa Uingereza linaendelea kuwaondoa watalii raia wa nchi hiyo mjini Mombasa kufuatia madai kwamba eneo hilo sio salama.

https://p.dw.com/p/1C19J
Picha: Getty Images

Hatua hii imechukuliwa baada ya ofisi ya mambo ya kigeni ya Uingereza kusema raia wake lazima waondoke kutokana na vitisho vya mashambulizi ya kigaidi. Tayari watalii hao wameanza kuondoka mjini humo huku baadhi ya washikadau wa sekta ya utalii wakisema hatua hio huenda ikayumbisha sekta hiyo nchini Kenya. Kupata zaidi juu ya hayo Amna Abubakar amezungumza na meneja wa hoteli moja mjini Mombasa Daudi Nyamu na kwanza anaelezea juu ya athari za hatua hiyo iliochukuliwa na shirika la usafiri la Uingereza. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman