1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Wakaazi wa bonde la mto wa Nairobi wahamishwa

29 Julai 2009

Wapiganaji wa Haki za Binadamu wa Kimataifa wameitaka serikali ya Kenya kuwapatia makaazi mapya watu 3,000 waliohamishwa kwa nguvu kutoka bonde la mto wa Nairobi ili kujenga barabara mpya na pia kuusafisha mto huo.

https://p.dw.com/p/Izhm
Hadi watu 127,000 wako katika hatari ya kulazimishwa kuhama kutoka vibanda vyao wanamoishi na kufanya biashara. Othman Miraji alizungumza na Hassan Omar Hassan Kamishna katika tume ya Taifa ya Haki za Binadamu nchini Kenya, vipi anavyoitathmini hatua hiyo ya polisi. Mwandishi: Othman Miraji Mhariri: Mohamed Abdulrahman