1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Wanajeshi watatu wa GSU wajeruhiwa katika mji wa Garissa

28 Oktoba 2011

Mripuko huko kaskazini ya Kenya, karibu na mji wa Garissa, umewajeruhi leo wanajeshi watatu wa GSU.

https://p.dw.com/p/131G8
Jeshi la nchini KenyaPicha: dapd

Gari ambamo wanajeshi hao walikuwa wakisafiria liliharibika vibaya sana na kwa sehemu iliungua baada ya kugonga kile polisi wanashuku huenda ni bomu la kutega ardhini au bomu la kawaida,

Wakati huohuo, mwananchi wa Kenya alipatikana na hatia na mahakama ya Nairobi leo kwa kufanya shambulio la grenedi katika mji huo wiki hii, na kuwa mwanachama wa kikundi cha waislamu wenye siasa kali nchini Somalia, al-Shabaab. Alipewa hukumu ya kifungo cha maisha gerezani kwa kufanya shambulio hilo, miaka 15 kwa kuwa mwanachama wa al-Shabaab, na miaka saba kwa kuwa na magrenedi na bunduki kinyume na sheria.

Othman Miraji alimuuliza , kwa njia ya simu , wakili wa mjini Mombasa, Aboubakar Yusuf, anavoitathmini hukumu hiyo...

Mwandishi: Othman Miraji

Mhariri: Josephat Charo