1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yatamba Osaka

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTO

MWISHOE:OSAKA:

Kenya imemaliza nafasi ya pili nyuma ya dola kuu Marekani katika mashindano ya ubingwa wa riadha ulimwenguni mjini Osaka,Japan yaliomalizika leo:

Baada ya Cathrine Ndereba kuipatia Kenya medali ya dhahabu katika mbio za marathon mapema hii leo, Alfred yego alishinda mbio za mita 800 kwa muda wake wa dakika 1:47.09.

Mkenya mwengine aliechukua uraia wa Marekani Bernard Lagat,bingwa tayari wa mita 1500 katika mashindano haya, alimvua leo ubingwa Eluid Kipchoge wa Kenya halisi na kutoroka na medali ya pili ya dhahabu katika finali ya mita 5000.Amekuwa mwanariadha 3 tangu Paavo nurmi wa Finland na El Gerouj wa Morocco kufanya hivyo.

Kenya imeipiku Urusi na kuchukua nafasi ya pili katika orodha ya medali nyuma ya Marekani.Ethiopia imekuja nafasi ya 4 nyuma ya Urusi.