1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yateketeza marundo ya pembe za tembo

30 Aprili 2016

Rais wa Kenya Jumamosi (30.04.2016) amechoma maelfu ya pembe za ndovu na faru na kuteketeza mrundiko wa pembe hizo na kutuma ujumbe mkali kwamba biashara ya viungo vya wanyama haina budi kukomeshwa.

https://p.dw.com/p/1Ifor
Picha: picture-alliance/dpa/D.Kurokawa

Moshi ulitanda wakati mrundiko wa pembe hizo ukiteketea katika mbuga ya wanyama ukingoni mwa mji mkuu wa Nairobi na kuangamiza tani 105 za pembe kutoka takriban wanyama 8,000 ambao ni uchomaji mkubwa sana wa aina yake.

Rais Uhuru Kenyatta amepuuzilia mbali hoja za wale walioitaka Kenya ambayo ilichoma pembe zake za kwanza hapo mwaka 1989 badala yaake ingeziliuza pembe hizo ambazo zinakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 150.

Alisema kabla ya kutia moto rundo la kwanza la pembe hizo kati karibu ya marundo kumi na mbili kwamba "Kenya inatowa ujumbe kwamba kwa sisi pembe haina thamani venginevyo inakuwepo kwa tembo wenyewe."

Kenya yataka marufuku ya pembe

Kenya itataka kupigwa marufuku kabisa kwa mauzo ya pembe duniani wakati wa Mkutano juu ya Biashara ya Kimataifa kwa Wanyama na Mimea ilioko hatarini kutoweka iliopangwa kufanyika Afrika Kusini baadae mwaka huu wakati ujangili ukizidi kuhatarisha wanyama hao.

Pembe zikiteketezwa Kenya. (30.04.2016)
Pembe zikiteketezwa Kenya. (30.04.2016)Picha: Getty Images/AFP/C. de Souza

Mkutano huo wa CITES ulipiga marufuku biashara ya pembe za tembo wa Afrika hapo mwaka 1989 lakini baadae iliruhusu mauzo.

Wito wa Kenyatta wa kupigwa marufuku kwa pembe za tembo umeungwa mkono na Rais Ali Bongo wa Gambia maskani ya tembo wa msituni.

Bongo amesema "kwa majangili wote ,kwa wanunuzi wote, kwa wafanyabiashara wote siku zenu zimemalizika."

Maruku hupunguza mahitaji

Watetezi wa mazingira wamesema marufuku ya awali ya CITES na uchomaji moto wa pembe hizo na Kenya hapo mwaka 1989 kumesaidia kupunguza mahitaji na kutowa faraja kwa tatizo hilo lakini mara baada ya kuruhusiwa mauzo halali jambo hilo limefufuwa soko lake.

Marundo ya pembe kabla ya kutiwa moto.
Marundo ya pembe kabla ya kutiwa moto.Picha: Reuters/T. Mukoya

Uwindaji haramu ilipamba moto kwa miaka mitatu hadi hapo mwaka 2012 wakati takriban tembo 100,000 waliuwawa sawa na kama tembo 33,000 kwa mwaka.

Katika miaka ya 1970 Afrika ilikuwa na kama tembo milioni moja na laki mbili lakini hivi sasa ina tembo 40,000 hadi 450,000.

Hali ya faru ni mbaya

Hali ya faru ni mbaya zaidi.Waliobakia Afrika hawazidi 30,00 na jamii moja inayotambulika kama "Faru Mweupe wa Kaskazini " wako katika hatari ya kutoweka.Faru hao watatu waliobakia wanahifadhiwa chini ya ulinzi mkali nchini Kenya.

Faru mweupe wa kaskazini alioko hatarini kutoweka.
Faru mweupe wa kaskazini alioko hatarini kutoweka.Picha: picture-alliance/AP Photo/L. Ignelzi

Kenya inategemea utalii ambapo wengi huvutiwa katika kambi za kifahari kutokana na wanyama mashuhuri watano ambao Kenya inajivunia :tembo,faru,chui,simba na nyati.

Ahadi zilizolewa na China na Marekani mwaka jana ambazzo ni masoko makuu mawili ya pembe za kuweka marufuku ya moja kwa moja ya kuagizia na kusafirisha pembe zimesaidia kuangusha bei za pembe.

Lakini bei za pembe za faru bado zinaendela kupanda. Doria za askari wa wanyama pori wenye silaha katika hifadhi na hatua nyengine zimesaidia kudhibiti uwindaji haramu kwa kiasi fulani lakini mustakbali wa mnyama huyo bado uko hatarini.

Katika miaka ya 1970 Kenya ilikuwa na faru 20,000 na kupunguwa hadi kufikia 400 katika miaka ya 1990.Hivi sasa ina takriban faru weusi 650 na inawahifadhi faru weupe watatu wa kaskazini wakati wanasayansi wakishindana na wakati kutafuta mbiu ya kuwapandikiza uzazi.

Mwandishi : Mohamed Dahman/Reuters

Mhariri : Daniel Gakuba