1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi dhidi ya raia wa Ufaransa kwa kudaiwa kuwateka nyara watoto 103 yaanza nchini Tchad

21 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cehj

NDJAMENA:

Raia 6 wa kifaransa wanaofanya kazi za utoaji misada na kushtumiwa kuwateka nyara watoto 103 wanasimama kizimbani Ijumaa.Watu hao ni watumishi wa shirika la kiutu linaloitwa Zoe’s Ark na walikamatwa mwisho wa mwezi wa Oktoba wakijaribu kuwasafirisha watoto hao kutoka Tchad hadi Ulaya. Washukiwa wanadai kuwa walikuwa wanawahamisha mayatima wa Darfur kwa famila za Ulaya,ingawa uchunguzi unaonyesha kuwa hakuna kati ya watoto hao aliekuwa yatima wala kutoka mkoa wa matatizo wa Darfur nchini Sudan.