1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi dhidi ya Taylor yafunguliwa tena

7 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/ClDV

THE HAGUE

Kesi ya Uhalifu wa kivita dhidi ya aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor inafunguliwa tena hii leo ikiwa ni miezi sita baada ya kufanyika kikao kilichogubikwa na rabsha nyingi.

Katika kikao cha leo mtaalamu juu ya biashara ya kimataifa ya madini ya almasi atakuwa mtu wa kwanza kutoa ushahidi wake mbele ya mahakama hiyo.Taylor mwenye umri wa miaka 59 anatuhumiwa kwa kuwatendea kinyume wananchi wa Sierra Leone kwa kuchochea mauaji yaliyofanywa na waasi waliokuwa wakiwakatakata watu viungo vya mwili katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 10.Taylor anakabiliwa na mashatka 11 ya uhalifu wa kivita ikiwa ni pamoja na mauaji,ubakaji,na kuwaingiza watoto jeshini.Taylor anayekanusha mashtaka yote 11 ni kiongozi wa zamani wa kwanza barani Afrika kuwahikufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita.