1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya Kenyatta katika ICC yaangaziwa zaidi

10 Oktoba 2014

Gazeti la mrengo wa kushoto la Tages Zeitung linalotoka mjini Berlin, lilikuwa na makala wiki hii kuhusu kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuhusiana na uhalifu dhidi ya binaadamu

https://p.dw.com/p/1DT3N
Uhuru Kenyatta Kenia Präsident
Picha: Reuters/Peter Dejong

Hii ni kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu desemba 2007 nchini mwake. Wiki hii Uhuru alifika mbele ya mahakama hiyo kama alivyotakiwa na Tages Zeitung likaandika :-

Akiwa rais wa kwanza aliyeko madearakani, Kenyata alifika The Hague ambako kulishuhudiwa mabishano ya hoja kati ya waendesha mashtaka na upande wa utetezi. Kenyatta mwenyewe hakusema lolote mahakamani. Kenyatta angeweza kukaidi na kubakia nyumbani, lakini alitaka kuonyesha anaondoka kwenda Hague kifua mbele na kuonyesha kwamba kesi hiyo imeshindwa hata kabla haijaanza.

Inadaiwa Kenyatta alikuwa muandalizi mshirika wa kundi la wanamgambo wa Kikikuyu la Mungiki. Itakumbukwa fujo zilizozuka baada ya uchaguzi huo zilisababisha watu karibu 1,300 kuuwawa

Wakili mkuu wa Kenyatta alisema hakuna usahidi na akataka ifutwe na kwamba serikali ilishirikiana vya kutosha na mahakama.

Waendesha mashtaka lakini wamedai Kenya imeshindwa kutoa ushirikiana kama inavyohitajika na hilo limevuruga ushahidi uliokuwa ukikusanywa. Lini jopo la majaji utatoa uamuzi wake kama iendelee au ifutwe haijulikani. Kwa sasa kilichojitokeza ni kwamba Kenyatta alitaka baada ya kikao hicho kuruka usiku kurudi nyumbani kusherehekea kile anachokiona ni ushindi kwake.

Uhuru Kenyatta Empfang in Kenia 9. Oktober
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto baada ya kurejea nchini kutoka The HaguePicha: Reuters/Noor Khamis

Süddeutsche Zeitung nalo lilikuwa na uhariri kuhusu kisa cha Uhuru Kenyatta, likiandika, sio hata rais aliyemadarakani anayeweza kukimbia sheria. Hilo linaonekana katika kesi dhidi ya Kenyatta. Lakini Rais huyo wa Kenya ameuhujumu utaratibu wa kesi hiyo. Süddeutache Zeitung linasema jumuiya ya kimataifa haipaswi kuruhusu kitu kama hicho. Serikali ya Kenyatta imekuwa ikifuja uchunguzi wa mahakama tokea 2013 kwa kukata kuwasilisha nyaraka zilizotakiwa. Mchakato wa kesi hiyo unakabiliwa na hatari ya kuporomoka.

Jumuiya ya kimatifa imetaka kuonyesha hakuna anayeweza kufanya maovu bila ya kuadhibiwa- hata viongozi, la sivyo mchakato mzima wa mahakam hiyo ya kimataifa utasita, pasiwepo na hali ya kulindwa kwa masilahi ya watu wachache wenye nguvu na kukandamizwa maadili ya kuheshimu sheria ya kimataifa..

Gazeti la Berliner Zeitung , lilikuwa na makala kuhusu “ ripoti ya Takwimu,” kama ilivyoitwaa, kuhusu sera ya msaada wa maendeleo ya serikali kuu ya mungano kati ya chama cha SPD na CDU/CSU. Gazeti hilo linasema takriban hakuna kifungu kisichoambatana na ukweli wa mambo katika suala hilo. Hadi 2015 inakusudia kuendelea na jukumu lake hilo la kimataifa kuhusiana na msaada wa maendeleo kwa kubakia kwenye kiwango cha alao 0.7 asili mia ya pato lake la uchumi. Ujerumani inalenga kuongeza msaada wake mwa maendeleo maradufu.

Südafrika Chinesische Investionen FAW Autowerk
Suala la Maendeleo barani Afrika pia limejadiliwa katika magazeti ya UjerumaniPicha: Imago

Lakini vipi inaziangalia nchi zenyewe zinazoendelea ? mataifa ya Kiafrika yamejitolea yenyewe kulipa msaada wa nchi za magharibi kupitia mikataba ya kimataifa, kwa njia ya kutenga sehemu fulani ya bajeti zao katika sekta za huduma ya afya. elimu na kilimo , ili kuboresha maisha ya watu wao. Shirika la misaada ya maendeleo linalojulikana kama ONE linasema hata hivyo kwamba kujitolea huko kwa mataifa ya kiafrika hakulingani na mahitaji ya Ulimwengu wa magharibi.

Kwa mujibu wa utafiti wa 2011 -2012 ni nchi 6 tu kati ya 43 za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara, ambazon zimetimiza wajibu wao kwa kutumia asili mia 15 ya bajeti zao za taifa katika huduma ya afya. Hali pia si nzuri katika kilimo .Hapa ni nchi 41 zilizoahidi kuwajibika lakini ni 8 tu zilizoekeza katika sekta hiyo. Ahadi hizo zilikuwa za 2008-2010.

Ripoti inasema hali ni mbaya katika elimu pia. Sababu kubwa ni mapato madogo ya kodi na kupotea kwa mapato ya serikali kwa sababu ya rushwa na usafirishaji fedha nje kinyume cha sheria. Nchi nne zimetajwa kuwa nyuma zaidi katika elimu nazo ni Jamhuri ya Afrika kati, Niger, Madagascar na jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Gazeti la Frankfurter Allgemeine limegusia juu ya shughuli za kibiashara barani Afrika. Baara ambalo uchumi wake umekuwa takriban kila mwaka kwa zaidi ya miaka 15 iliopita katika kiwango cha jkaribu asili m ia 5. Haya yanatokana na uatafiti uliofanywa na takriban makampuni 400 ya Kijerumani chini ya Jumuiya inayoratibu wafanya biashara na wawekezaji KPMG. Hata hivyo Tim Lobig , kutoka kampuni ya washirika na mtaalamu wa Afrika katika kampuni ya mahesabu na ushauri, anasema huenda kuna nafasi nyingi zisizogunduliwa Afrika na kinachoripotiwa ni kile tu ambacho wafanyabiashara wamenufaika nacho. Hata hivyo linaandika Frankfuter Allgemeine Zeitung taarifa nyingi hazilengi ukweli wa mambo panapohusika na soko. Pia unaonekana ushindani mkubwa baina ya nchi za magharibi zilizoeneelea kiviwanda na China. Hata hivyo Löbig anasema sekta ambayo kijadi imebakia yenye nguvu yaani uhandisi na viwanda vya magari pamoja na nishati zinaonekana kuendelea kuwa na mafanikio. Pakisisitizwa juu ya haja ya kuimarishwa sekta muhimu, inaelezwa kwamba kwa kipindi cha miaka 35 ijayo, idadi ya wakaazi barani Afrika inatarajiwa kuongezeka wengi wakiendelea kuishi mijini. Kutokana na hayo kuna haja kubwa ya kuimarishwa mambo muhimu kama barabara, shule na hospitali.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman/ Dt Zeitungen
Mhariri: Yusuf Saumu