1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya Mladic yaahirishwa

17 Mei 2012

Kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili Kiongozi wa zamani wa Jeshi la Bosnia, Ratko Mladic, imeahirishwa kwa muda usiojulikana kutokana na upande wa mwendesha mashitaka kukiuka taratibu za mashitaka.

https://p.dw.com/p/14x91
Ratko Mladic
Ratko MladicPicha: picture-alliance/dpa

Maamuzi hayo yamefikiwa na Jaji Alphons Orie katika mahakama ya uhalifu wa Kivita ya mjini The Hague juu ya uhalifu uliofanyika katika taifa hilo na Mladic.

Maamuzi hayo yamefikiwa mara baada ya upande wa mwendesha mashitaka kuonyesha shimo katika mauaji hayo kwa Waislamu wa Bosnia Serbia ya mwaka1995 katika eneo la Srebrenica ambayo yanaaminika kuandaliwa na Mladic yakiaminika kuwa ya kutisha tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.

Mladic akifahamika kama muuwaji wa Bosnia anatuhumiwa kwa makosa dhidi ya binadamu na mauaji ya haraki ya kati ya mwaka 1992-1995 katika eneo la Balkar ambapo waislamu zaidi 8000 wakiwamo wanaume na wavulana wadogo waliuwawa.

Ratko Mladic akiwa mahakamani
Ratko Mladic akiwa mahakamaniPicha: dpa

Huku akituhumiwa moja moja kwa yeye mwenyewe kuwepo katika uwanja ambapo tukio hilo lilifanyika. Inadaiwa alifika na kuwapongeza askari wake kwa kutekeleza jukumu alilowapa, anasema Peter McCloskey kutoka upande wa mashitaka.

Mauaji ya watu laki moja

Katika mkanda maalumu wa video unamuonyesha Mladic akisema mauaji hayo yalikuwa zawadi kwa Waserbia. Upande wa mashtaka unadai kuwa Mladic aliyaandaa mauaji hayo ya halaiki. Katika nia yake ya kuwamaliza waislamu hao ambapo katika vita vya mwaka 1992-1995 watu zaidi ya 100,000 waliuwawa na milioni 2.2 waliachwa bila ya makazi.

Mahakama ilionyeshwa picha za makaburi ya waliuwawa katika unyamani unaomlenga Mladic kufanya. Waendesha mashitaka wameongeza kuwa amri nyingi za kutekeleza udhalimu huo zilitolewa kwa mdomo lakini pia kuna ushahidi wa nyaraka kadhaa huku baadhi ya wasaidizi wa kiongozi huyo wa zamani wa Jeshi wamekubali kuja kutoa ushahidi wao dhidi yake katika tuhuma 11 zinamkabaili ambapo sasa taratibu zimekiukwa.

Mapema upande wa mashtaka ulisema kuwa utaithibitishia mahakama pasi na shaka katika kila tuhuma zinazomkabili Mladic kutoka kwa wahanga, ndugu wa wahanga hao ambao wengine walishuhudia tukio hilo na wengine kuona lilipokuwa linarushwa na televisheni ya Sarajevo wakati wa utekelezaji wa mauaji hayo.

Mladic mwenye miaka 70, Kamanda wa zamani wa Jeshi la Bosnia Sebia mapema kabisa amekana kuhusika katika mauaji hayo na kama mahakama itamtia hatiani basi anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha gerezani kama shauri lake litarudishwa mahakamani tena.

Upande wa mashtaka pia walionyesha ramani ya namna Yugoslavia iliyokuwa na makabila kadhaa huku waislamu waliuwawa wakiwa ni miongoni mwa Wasebia waliotakiwa kumalizwa kabisa likiwa miongoni mwa malengo la Mladic.

Mladic akamatwa nyumbani kwa nduguye

Baada ya kumalizika vita hivyo Mladic aliendelea kuwa kiongozi wa Jeshi la nchi hiyo hadi mwaka 2000 baada ya kuangushwa kwa Rais wa Serbia wa wakati huo Sloban Milosevic. Mladic alijificha tangu wakati huo hadi Mei 2011 ambapo alikamatwa nyumbani kwa ndugu yake huko Lazarevo.

Ratko Mladic
Ratko MladicPicha: REUTERS

Kinachosubiriwa ni lini shauri hilo litapelekwa tena mahakamani. Leo hii Miladic ameonekana akiwa na afya njema kuliko alivyokuwa anafika mahakamani kwa mara ya kwanza.

Mwandishi: Adeladius Makwega/AFPE

Mhariri: Josephat Charo