1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Afisa aituhumu serikali mauaji ya halaiki

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeQ

Afisa wa ngazi ya juu,wa chama cha SPLM cha Sudan kilichojiunga katika serikali ya umoja wa taifa kufuatia makubaliano ya amani ya mwaka 2005, ameituhumu Khartoum kuhusika na mauaji ya halaiki na safisha-safisha ya kikabila.Pagan Amun,alikuwa akizungumza siku ya kuadhimisha mwaka wa pili tangu kufariki kwa John Garang,aliekuwa kiongozi wa SPLM.Garang,alifariki katika ajali ya ndege nchini Uganda.

Amun ametamka hayo,siku moja baada ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa,kulaani rasmi safisha-safisha ya kikabila katika jimbo la Darfur.Baraza hilo limeikosoa serikali ya Sudan kwa kushindwa kuwafikisha mahakamani wanamgambo wanaohusika na mauaji hayo katika jimbo la mgogoro la Darfur.