1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Askari mmoja wa polisi auwawa Darfur

20 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXM

Watu waliokuwa wamejihani na silaha wamemuua askari mmoja wa polisi na kuwajeruhi wengine wanne katika shambulio dhidi ya kambi moja ya wakimbizi katika jimbo la Darfur.

Washambuliaji walikifyatulia risasi kituo cha polisi katika kambi ya al Salam kusini mwa Darfur, makaazi ya maelfu ya watu waliolazimika kuzikimbia nyumba zao wakati wa kipindi cha miaka minne ya machafuko katika jimbo la Darfur.

Gavana wa jimbo la Darfur Kusini, Farrah Mustafa, amethibitisha kuuwawa kwa askari huyo na kujeruhiwa kwa wengine wanne.

Aidha kiongozi huyo amedokeza kuwa wanaume 26 walikishambulia kituo hicho na kujaribu kuiba magari ya polisi lakini wakashindwa. Uchunguzi unaendelea kuwasaka waliofanya shambulio hilo.