1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum. Jeshi la serikali lashutumiwa.

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HE

Kundi moja la waasi katika jimbo la Darfur nchini Sudan linaripotiwa kuwa limelishutumu jeshi la serikali ya Sudan kwa kuwauwa watu 40 katika shambulio dhidi ya mji mmoja unaodhibitiwa na waasi hao. Jeshi la Sudan Liberation Army ni kundi pekee la waasi lililotia saini makubaliano ya amani na serikali mjini Khartoum. Hali inayozidi kuwa mbaya ya ghasia kabla ya mazungumzo ya amani yanayotarajiwa kufanyika katika mji mkuu wa Libya, Tripoli , Oktoba 27.

Waziri wa Uingereza anayehusika na masuala ya Afrika Lord Malloch Brown ameyaonya makundi ya waasi yanayotishia kutohudhuria mkutano huo kwamba watapoteza haki yao ya kuhusika katika majadiliano ya amani.