1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Mapigano kusini mwa Sudan yameua watu 150

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCn7

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa amesema,zaidi ya watu 150 wameuawa na wengine 400 wamejeruhiwa vibaya nchini Sudan katika mapigano ya siku kadhaa,kati ya vikosi vya serikali na waasi katika mji wa kusini Malakal.Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan imeonya kuwa maiti zinazoelea katika Mto wa Nile zinachafua chanzo cha maji ya kunywa ya mji huo.