1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM : Mazungumzo ya Somali bado mashakani

1 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCxI

Wanadiplomasia wako mbioni kuokowa mazungumzo kati ya ujumbe wa serikali ya mpito ya Somali na Uongozi wa Kiislam kujaribu kuwashawishi nani anayepaswa kuwa mwenyekiti wa mazungumzo hayo na kuiepusha nchi hiyo na vita.

Wajumbe wa pande hizo mbili wako Khartoum lakini bado kukutana ana kwa ana kutokana na uongozi wa Kiislam kupinga kuwepo kwa majeshi ya Ethiopia nchini Somali na Kenya kushirikiana uenyekiti wa mazungumzo hayo na Umoja wa Waarabu.

Wajumbe wa pande hizo mbili wamejichimbia kwenye vyumba vya hoteli na hadi hivi sasa wanagoma kwenda kwenye ukumbi wa mkutano.