1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Serikali ya Sudan na waasi wakubali kusitisha uhasama kwa siku sitini.

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbl

Afisa mmoja mkuu wa Marekani amesema serikali ya Sudan na waasi wamekubali kusitisha uhasama kwa siku sitini katika eneo la Darfur lenye mzozo.

Gavana wa Jimbo la New Mexico, Bill Richardson, aliyekuwa nchini Sudan kwa ziara ya siku nne, amewaambia waandishi wa habari kwamba Rais wa Sudan, Hassan Omar al-Bashir amekubali yaanzishwe tena mashauriano ya amani.

Bill Richardson amesema viongozi wa waasi wanaunga mkono mwafaka huo utakaoanza kutekelezwa katika tarehe itakayotengwa na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika, AU.
Mzozo wa muda wa miaka minne katika Darfur umesababisha vifo vya watu kiasi laki mbili na wengine zaidi ya milioni mbili kupoteza makazi yao.