1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum. Serikali yamshutumu katibu mkuu.

26 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVw

Sudan imemshutumu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon jana Jumamosi kwa kulishutumu jeshi la Sudan kwa kutoondoa majeshi yake yote kutoka maeneo ya kusini mwa nchi hiyo kama yanavyotakiwa na makubaliano ya amani ya mwaka 2005. Makubaliano hayo yalimaliza miaka 21 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya upande wa kaskazini na kusini na kueleza kuwa jeshi la Sudan litaondoa wanajeshi wake ifikapo Julai 9, muda ambao Ban Ki-moon amesema katika ripoti siku ya Alhamis kuwa haukufuatwa.

Wakati huo huo serikali ya Sudan imelishutumu shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International kuwa limekuwa chombo cha ujasusi cha mataifa ya magharibi.

Balozi wa Sudan katika umoja wa mataifa Abdalhalim Abdalmahmud amelitaka shirika hilo kuomba radhi kwa kuishutumu Sudan kuwa inakiuka vikwazo vya umoja wa mataifa vya silaha.

Tumesikitishwa kuwa Amnesty International sasa imekuwa chombo cha ujasusi cha mataifa ya magharibi.

Imepoteza uhalali wale , na hilo linatusikitisha. Tunaangalia shughuli za shirika hilo na inaonekana wazi kwetu kuwa ni sehemu ya sauti zinazojirudia nchini humo kile ambacho mataifa ya magharibi yanasema juu ya nchi hiyo na hii kitaaluma na kiroho sio sahihi.