1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum. Sudan huenda ikakubali majeshi ya umoja wa mataifa.

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgs

Serikali ya Sudan imeonyesha ishara ya kuwa tayari kulikubali jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani katika jimbo la Darfur. Umoja wa mataifa umetoa ahadi ya kuweka jeshi la pamoja ambalo litajumuisha pia majeshi ya umoja wa Afrika katika jimbo hilo lililokumbwa na vita.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan anamatumaini kuwa rais wa Sudan Omar el Bashir atakubali huenda kuazia leo kusitisha mapigano kabisa na hatimaye kuwekwa kwa jeshi hilo la kulinda amani.

Wanajeshi 7,000 wa jeshi la umoja wa Afrika la kulinda amani limekuwa katika jimbo la Darfur katika muda wa mwaka mmoja uliopita, lakini hali ya machafuko inaendelea katika eneo hilo.