1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Sudan kutia saini makubaliano ya amani

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2w

Serikali ya Sudan na waasi kutoka mashariki mwa nchi wanatazamia kutia saini makubaliano ya amani kumaliza uasi wa chini kwa chini uliodumu mwongo mmoja katika eneo la mashariki lenye utajiri wa rasli mali.Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan na ujumbe wa maafisa wa ngazi ya juu watakwenda nchi jirani ya Eritrea iliyokuwa mpatanishi.Haya ni makubaliano ya amani ya tatu kujadiliwa na Khartoum katika muda usiozidi miaka miwili. Mashariki mwa Sudan,kuna utajiri wa madini ya dhahabu,almasi na pia kuna bandari pekee ya nchi hiyo.Port Sudan inatumiwa kusafirisha mafuta ya Sudan katika nchi za nje.Licha ya utajiri huo, eneo hilo la mashariki ni miongoni mwa maeneo masikini kabisa nchini Sudan.