1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Sudan yazionya nchi zitakazotuma majeshi Darfur

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5c

Sudan imetuma barua kwa nchi za Umoja wa Mataifa ambazo huenda zichangie wanajeshi wake katika jeshi la umoja huo la kulinda amani katika jimbo la Darfur.

Katika nyaraka hizo Sudan inasema itakichukulia kitendo hicho kuwa cha kikatili na chanzo cha uvamizi.

Kufuatia hatua hiyo ya Sudan baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa likikutana faraghani kulijadili swala hilo. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, John Bolton, ameikosoa Sudan kwa kutilia shaka mamlaka ya umoja huo, akisema barua ya Sudan haijawahi kuandikwa na taifa lolote na haina msingi.

Tume ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika iliyo na wanajeshi 7,000 imeshindwa kukomesha machafuko katika eneo la Darfur, kati ya waasi na wanamgambo wa janjaweed, wanaoungwa mkono na serikali ya Sudan.