1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Tume ya Umoja wa Mataifa kukutana na Rais wa Sudan

17 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBr2

Tume ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, imewasili Khartoum,mji mkuu wa Sudan,kukutana na Rais Omar al-Beshir.Tume hiyo inataka hakikisho kutoka Rais al-Beshir juu ya njia ya kutekeleza makubaliano ya kupeleka vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika,katika jimbo la mgogoro la Darfur,magharibi mwa Sudan.Khartoum ambayo hapo awali ilipinga juhudi za kupeleka vikosi vya kimataifa kulinda amani Darfur,juma lililopita lilibadilisha msimamo wake kufuatia shinikizo kubwa la kimataifa na vitisho vya kuwekewa vikwazo vikali na Umoja wa Mataifa.Hivi sasa,kama wanajeshi 7,000 wa Umoja wa Afrika wapo Darfur,lakini hawakuweza kuzuia mapigano.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,hadi watu 200,000 wamepoteza maisha yao katika mgogoro huo wa miaka minne.Vile vile,zaidi ya watu milioni mbili wamelazimishwa kuondoka majumbani mwao.