1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM : Waasi wa zamani wa kusini wajitowa serikalini

11 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gf

Waasi wa zamani wa kutoka chama cha Ukombozi wa Wananchi wa Sudan SPLM leo kimesitisha ushiriki wao kwenye serikali ya taifa kutokana na serikali hiyo kushindwa kutekeleza makubaliano ya amani.

Uamuzi huo umefikiwa wakati wa mkutano uliofanyika leo hii mjini Juba chini ya uenyekiti wa mkuu wa chama cha SPLM Salva Kiir.Imeelezwa kwamba chama hicho kimewaita nyumbani mawaziri wake wote na washauri wa rais.

Chama hicho kinasema serikali mjini Khartoum imeshindwa kutekeleza vifungu vingi vya makubaliano ya mwaka 2005 ya kushirikiana madaraka na utajiri kati ya serikali ya taifa na serikali ya utawala wa ndani kusini mwa Sudan.