1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Watoto wanatumiwa kupigana vita Darfur

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVw

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Darfur, Radhika Coomaraswamy,amelalamika kuwa watoto wengi wanalazimishwa kuingia jeshini kupigana katika jimbo la mgogoro la Darfur nchini Sudan. Coomaraswamy,ametoa taarifa yake mjini Khartoum baada ya kufanya ziara ya kujionea mwenyewe hali kama ilivyo katika eneo hilo la mgogoro,magharibi mwa Sudan.Tangu mwanzo wa mwaka 2003 wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Khartoum wanapigana na waasi katika jimbo la Darfur.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,zaidi ya watu 200,000 wameuawa katika mgogoro wa Darfur.