1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum yashindwa kutimiza ahadi ya majeshi yake kusini mwa Sudan kama ilivyotakiwa

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjSv

JUBA:

Utawala wa Khartoum umeshindwa kutimiza ahadi yao ya kuondoa vikosi vyao katika eneo la Sudan Kusini.

Kamanda wa juu wa waasi wa zamani wa Sudan Peoples Liberation Army-SPLA- amesema hii inaifanya serikali kuvunja mkataba ambao uliwafanya waasi kujiunga tena na serikali.

Major Generali Mai Hoth,ambae ni naibu mkuu wa utawala katika jeshi la Sudan Kusini,amesema kuwa aksari hao hadi sasa hajaondoka na bila kutoa sababu maalum. Kuondoka kwa majeshi ya Khartoum kutoka maeneo ya kusini mwa nchi hiyo ni sehemu ya mapatano ya mwaka jana ambapo wapiaganaji wa SPLA walijiunga katika serikali ya muungano disemba 27.

Mgogoro wa SPLA kujiondoa katika serikali ulidumu miezi miwili.Sababu moja wa waaasi hao wa zamani kujiondoa katika serikali ilikuwa kushindwa kwa utawala wa Kahartoum kuondoa askari wake kutoka sehemu za kusini mwa nchi hiyo.