1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum.Egeland aionya zaidi serikali ya Sudan juu ya Darfur.

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqA

Mkuu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Jan Egeland ameishutumu Serikali ya Sudan kuwa ndio inayosababisha hali kuwa mbaya huko Darfur.

Egeland amesema raia wa Sudan milioni nne katika jimbo la Darfur wamekata tamaa ya kupata misaada ya kiutu.

Aidha ameonya kwamba nchi hiyo inaweza ikakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa misaada hadi pale hatua za kweli za kusimamisha matumizi ya silaha zitakapochukuliwa na kufikia makubaliano ya amani.