1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Sudan yakubali Umoja wa Mataifa uweke majeshi Darfur?

16 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9X

Sudan imetia saini mapatano kuruhusu majeshi ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kuwekwa katika jimbo la Darfur.

Mapatano hayo yamefikiwa kutokana na usuluhishi uliofanyika wakati wa mkutano wa viongozi wa Umoja wa nchi za kiarabu mjini Riyadh hivi karibuni.

Habari zinasema Umoja wa Mataifa unakaribia kufikia mapatano na Sudan juu ya kuongeza wanajeshi alfu 3 pamoja na zana. Hatahivyo waziri wa mambo ya nje wa Sudan Lam Akol amesema kuwa nchi yake ipo tayari kuruhusu idadi yoyote ya askari wa Umoja wa Afrika lakini haitakubali wanajeshi wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur.