1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Waasi wahimizwa kuhudhuria mkutano wa Libya

22 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNe

Washiriki katika mkutano unaofadhiliwa na Umoja wa mataifa wanatoa wito kwa waasi wote wa darfur kuhudhuria mazungumzo muhimu ya kutafuta amani yanayopangwa kufanyika nchini Libya mwezi ujao.Kikao hicho kinalenga kumaliza mgogoro wa Darfur nchini Sudan.Ban Ki Moon katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

''Washiriki wote wanakubali kuwa mazungumzo hayo ya pande tatu yanayojumuisha mashirika ya Umoja wa mataifa,mashirika ya misaada na serikali yaendelee kwa pamoja.''

Waziri wa mambo ya kigeni wa Sudan Lam Akol anaelezea kikao cha jana kuwa na mafanikio na kusisitiza kuwa yoyote ambaye hatashiriki katika mazungumzo yajayo ya Tripoli,Libya atachukuliwa hatua kali.Kiongozi huyo anaongeza kuwa majeshi ya kulinda amaani yanayopangwa kwenda Darfur yanatosha

''Kuna majeshi ya kutosha kutoka mataifa ya Afrika.Mataifa ya Afrika yamechangia asilimia 190 ya majeshi yanayohitajika kwahiyo hakuna matatatizo.''

Kulingana na takwimu za umoja wa mataifa watu laki mbili wameuawa na wengine milioni 2 kuachwa bila makao katika vita hivyo vilivyodumu miaka minne.