1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Wawakilishi wa makundi saba ya waasi wanakutana

15 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fc

Wawakilishi wa makundi saba ya waasi katika jimbo la Darfur wanakutana kusini mwa Sudan kujadili uwezekano wa kufikia makubaliano ya kuwa na sauti moja kabla ya mkutano wa amani na viongozi wa serikali ya Sudan unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 mwezi huu nchini Libya.

Waandalizi wa mkutano huo unaofanyika mjini Juba mji mkuu wa Kusini mwa Sudan wamesema kua wawakilishi hao wana muda wa siku tano kufikia makubaliano.

Waandalizi hao wanatarajia kuwa muasisi wa kundi la waasi la SLM Abdel Wahed Mohamed el Nur atahudhuria mazungumzo hayo ya amani.

El Nur mara kwa mara amekuwa anakataa kuhudhuria mazungumzo yoyote ya amani kabla ya kwanza serikali ya Khartoum kukubali madai yake kadhaa.