1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiasi watu sita wauwawa katika shambulio mjini London

Sekione Kitojo
4 Juni 2017

Kiasi watu sita wameuwawa na zaidi ya 30 wanapatiwa matibabu katika  hospitali baada ya magaidi kuendesha gari na kuwagonga  wapita njia London na kisha kuwachoma visu watu katika baa katika usiku wa Jumamosi(03.06.2017)

https://p.dw.com/p/2e6T7
England Vorfall auf der London Bridge Mehrere Fußgänger angefahren
Watu walielekezwa kwenda katika eneo salama baada ya tukio la kigaidi mjini LondonPicha: Getty Images/C. Court

Washambuliaji watatu, ambao  walikuwa  wamevalia  mikanda  ya  bandia  ya  miripuko , pia walipigwa  risasi na  polisi  na  wamefariki, polisi  ya  mjini  London  imesema.

England Vorfall auf der London Bridge Mehrere Fußgänger angefahren
M;ajeruhi wakipelekwa hospitali baada ya tukio la kigaidi mjini LondonPicha: Picture alliance/empics/F. De Caria

"Katika  wakati  huu, tunaamini  kwamba  watu  sita  wameuwawa  pamoja  na  washambuliaji watatu waliopigwa  risasi  na  polisi," amesema  kamishna  msaidizi  Mark Rowley , ambae pia  ni  mkuu  wa  kitengo  cha  kupambana  na  ugaidi.

Washukiwa  waliwagonga  wapita  njia  katika  daraja  la  London  kabla  ya  kuwashambulia watu  katika  baa za  karibu  na  migahawa, Rowley  alisema. Polisi  wenye  silaha waliwapiga  risasi  washambuliaji  watatu  katika  muda  wa  dakika  nane   baada  ya  polisi kupokea  siku  ya  kwanza  ya  kuhusiana  na   mashambulio  hayo  ya  kigaidi  katikati  ya London  usiku  wa  Jumamosi, amesema.

Simu  ya  kwanza  ilipokelewa baada  ya  washambuliaji  kuendesha  gari  yao  na kuwagonga  wapita  njia  katika  daraja  la  London  kabla  ya  kuwachoma  visu watu  katika soko  la  karibu  la  Borough, Rowley  amesema.

England Vorfall auf der London Bridge Mehrere Fußgänger angefahren
Polisi wakilinda usalama katika eneo la tukio la kigaidi mjini LondonPicha: Getty Images/C. Court

Watu walioshuhudia  waliliambia  gazeti  la  Guardian waliwaona  watu  wawili wakiwachoma visu  watu  nje  ya  mgahawa  maarufu  wa  Roast  katika  soko  la  Borough. "Niliwaona  watu wawili  wakiwa  na  visu vikubwa  nje  ya  mgahawa  huo  wa  Roast," mpishi  kutoka  katika mgahawa  wa  karibu  aliliambia  gazeti  hilo.

Polisi wachukua  hatua ya  haraka

Walikuwa  wakiwachoma  visu  watu , tulikuwa  tunapiga  kelele "acha, acha"  na  watu walikuwa  wakiwatupia  viti," mpishi  huyo  alisema. "polisi walikuja  na  kuwapiga  risasi watu  hao moja  kwa  moja."

England Vorfall auf der London Bridge Mehrere Fußgänger angefahren
Watu ambao walipata mshituko baada ya tukio la kigaidi mjini LondonPicha: Reuters/H. McKay

Waziri  mkuu  Theresa  May  aliliita  shambulio  hilo  kuwa "tukio la kigaidi" na  alieleza "shukrani  zake nyingi" kwa  polisi  na  huduma  za  dharura. Meya  wa  London Sadiq Khan amesema  anapanga  kuhudhuria  mkutano mapema  leo Jumapili (04.06.2017) wa  kamati ya  dharura  ya serikali inayojulikana  kama  cobra, ambayo  inatarajiwa  kuongozwa  na waziri  mkuu  May.

"Mpaka  sasa  hatufahamu  maelezo  zaidi, lakini  hili  lilikuwa  shambulio  la  makusudi  na  la waoga dhidi  ya  wakaazi  wa  London ambao hawana  hatia  na  watu  wanaotembelea  mji wetu wakifurahia  usiku  wao  wa  Jumamosi," Khan  alisema.

Trump azungumza na  May

Rais donald Trump  amempigia  simu  waziri  mkuu  wa  Uingereza  Theresa May  na  kumpa rambi  brambi  zake  kufuatia tukio  la  kigaidi mjini  London.

England Vorfall auf der London Bridge Mehrere Fußgänger angefahren
Watu wakikimbia kutoka eneo la tukio mjini LondonPicha: Picture alliance/AP Photo/M. Dunham

Rais Trump  alizungumza  na  waziri  mkuu  May  leo  na  alitoa  rambi  rambi  zake  kwa shambulio  hilo  la  kinyama la  kigaidi katikati  ya  London.Trump  aliahidi  msaada  kwa Uingereza  kutokana  na  mashambulio  hayo  mawili  ya  kigaidi  ambapo  watu  sita waliuwawa , baada  ya   gari  kuwagonga  wapita  njia na  washambuliaji  hao  kuwachoma visu watu  kadha.

Katika  mazungumzo  yao  ya  simu  Trump  aliahidi  kwamba  Marekani  itatoa  ushirikiano kamili  kwa  Uingereza  katika  uchunguzi wa  tukio  hilo  na  kuwafikisha  watu  wanaohusika na  tukio  hilo  la kiuwoga  mbele  ya  sheria.

Justin Trudeau Kanada äußert sich zu London
Waziri mkuu wa Canada Justin TrudeauPicha: picture alliance/dpa/Canadian Press

Waziri  mkuu  wa  Canada  Justin Trudeau  amesema  kwamba  wacanada , "wanasimama pamoja  na Waingereza" baada  ya  washambuliaji  kuwachoma  visu holela  watu  na kuwagonga  wapita  njia kwa  gari na  kuuwa  watu  sita.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / dpae /

Mhariri: Bruce Amani